Tuesday, September 20, 2016

WANANCHI WATAKIWA KUZITUMIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA


Mkurugenzi wa idara ya maafa ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbaazi Msuya akizungumza na wanahabari wa Mwananchi na Majira Bertha Mollel na Pamela Mollel kwenye semina ya kuwajengea uwezo wanahabari mashirika ya serikali na yasio ya kiserikali juuu ya kutambua masuala ya Taadhari za Awali iliyofanyika kwenye hotel ya Lush Garden Wilayani Arumeru picha zote na Mahmoud Ahmad,Michuzi Blog Arusha.
Baadhi ya wawezeshaji wakiandaa Taarifa za kuwasilisha kwenye semina hiyo.

Washiriki wakifuatilia kwa makini mada ikiendelea .

Mwenyekiti wa semina hiyo Mery Mwita akiteta jambo na mratibu wa semina hiyo Clemence Maganga .
Wanahabari Kutoka Jambo leo na TV1 Wankyo Gati na Jeni Edward wakiendelea na kufuatilia mada katika semina hiyo ya kuwajendea uwezo wanahabari kutoka vyombo mbali mbali mkoani hapa kujua Masuala ya Maafa yakiwemo matetemeko, mafuriko na majanga mbali mbali na kufanyika wilayani Arumeru picha zote na Mahmoud Ahmad wa Michuzi Blog Arusha


Na Mahmoud Ahmad Arusha 
Watanzania wameshauri kuchukuwa tahadhari za awali zinazotolewa kabla na baada ya maafa na mamlaka mbali mbali za hali ya hewa hapa nchini na kote duniani kuweza kujianda na kuyakabili mabadiliko mbali mbali ya Tabianchi yanayoizunguka jamii. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi idara ya maafa ofisi ya waziri mkuu brigedia Jenerali Mbaazi Msuya wakati akifungua semina ya wanahabari, na mashirika ya serikali na yasio ya kiserikali kwa lengo la kuwa na uelewa wa kuchukuwa tahadhari ya kukabiliana na majanga na maafa yanapoweza kujitokeza hapa nchini ili baadae kutoa elimu kwa watanzania. 

Alisema jamii nyingi hapa nchini wamekuwa wakitoa taarifa mbali mbali juu ya matukio ikiwemo ya mvua,mafuriko kwa njia za kimila na matukio hayo kujitokeza na kushauri kuwa ifike mahali taarifa hizo zikafanyiwa kazi kwani zinakuwa zinaashiria ukweli . 

Alisema kuwa kupitia mafunzo haya yatawafanya waandishi wa habari hapa nchini kutambua vyanzo vya matukio na jinsi gani ya kuelimisha jinsi ya kukabiliana na maafa katika jamii kwani wengi wao wamekuwa wakiandika taarifa ambazo hawana uelewa nazo juu ya maafa ambayo yanajitokeza kama tetemeko la ardhi lililojitokeza hivi karibuni Mkoani Kagera. 

‘’Leo tumekuja kuwapa elimu waandishi wa Habari juu ya kuwa na uelewa wa taadhari mapema ya matukio na kukabiliana na majanga pamoja na maafa yanayotokea kutokana na muingiliano wa shughuli za kibinadamu sehemu mbalimbali hapa nchini’’alisema Brigedia jenerali Msuya. 

Aidha aliitaka jamii kote nchini kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia wenzao Mkoani Kagera ambao walipatwa na janga la Tetemeko la Ardhi kwa kuwapelekea mabati na Saruji ambavyo vitataua tatizo kuliko kuliko matenti ambayo yatakaa kwa muda mfupi na kutomaliza tatizo. 

Kwa upande wake Alfed Daniel ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa uboreshaji wa taarifa za hali ya hewa na uwezeshaji wa taarifa za taadhari za awali alisema kuwa lengo kubwa ni kutaka kuwajenga wanahabari na taasisis zisizo kuwa za kiserikali ili waweze kuwa na uelewa wa taarifa za taadhari awali za mifumo ya taarifa za taadhari za awali za hali ya hewa na kuweza kuzisambaza kwa walengwa jinsi gani waweze kuzitumia kwa muda kujikinga na majanga hayo. 

Alfred aliongeza kuwa kupitia mafunzo hayo yataenda kuleta tija kwa jamii huku akiwasihi wananchi kuzifanyia kazi taarifa mbalimbali ambazo zinatakuwa zikitolewa na wataalamu na vyombo vya habari hapa nchini jambo ambalo litasaidia kuondokana na kupata athari kubwa pindi matukio hayo yanapotokea.


Post a Comment