Wednesday, September 28, 2016

TRA YAIBUKA TAASISI YENYE UWAZI ZAIDI MIONGONI MWA TAASISI ZA UMMA NA KUWA KINARA NA KUNYAKUA TUZO YA MISA-TAN YA UFUNGUO WA DHAHABU

Afisa wa TRA akiwa amepokea tuzo ya Taasisi iliyonyakuwa tuzo ya dhahabu kwa kuwa taasisi yenye uwazi zaidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Balozi wa Jumuiya ya Ulaya-Tz Roeland Van de Gree, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa akifuatiwa na Afisa Utafiti na Maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa na kulia ni Rais mstaafu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya.

Afisa Utafiti na Maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa (wa kwanza kushoto) akionyesha akikabidhi tuzo ya kufuli kwa taasisi iliyoongoza kwa usiri katika utoaji taarifa kwa Balozi wa Jumuiya ya Ulaya-Tz Roeland Van de Gree ili aikabidhi kwa Taasisi iliyonyakua tuzo hiyo ya Wizara ya Wizara ya Sheria na Katiba.

Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia shughuli nzima iliyokuwa inaendelea wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Millenium Seashells jijini Dar es salaam leo.Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.
 Afisa habari Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Edith Nguruwe na Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Nasra Abdallah wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye siku ya kimataifa ya uhuru wa Kujua.
 Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia shughuli nzima iliyokuwa inaendelea wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Millenium Seashells jijini Dar es salaam leo.Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.
 Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia shughuli nzima iliyokuwa inaendelea wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Millenium Seashells jijini Dar es salaam leo.Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa, Afisa Utafiti na Maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa (wa kwanza kushoto) akionyesha ripoti iliyozinduliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa chapisho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini, kushoto ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya-Tz Roeland Van de Gree ambao ni mmoja wa wadhamini wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, na kulia ni Rais mstaafu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba nchini, Amon Mpanju akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,Wahariri,Viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini na taasisi mbalimbali wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Seashells jijini Dar es salaam leo.Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.Pamoja na mambo mengine Mpanju alisema serikali haiungi mkono ndoa za jinsia moja na kuwataka wadau kuungana kupiga vita ndoa hizo ambazo kwa mujibu wa sheria na tamaduni za kitanzania hazikubaliki.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza jambo kwa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa klabu za waandishiwa habari (press clubs) wa mikoa mbalimbali waliokutana kujadili changamoto wanazozipata pamoja na kujadili rasmu ya sheria mpya itakayopitishwa bungeni hivi karibuni.

 Rais mstaafu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya akiwaomba viongozi wa press club waliofika katika mkutano uliokuwa ukijadili mswada wa sheria mpya ya vyombo vya habari
Baadhi ya viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.

No comments: