Monday, September 26, 2016

SPIKA JOB NDUGAI ATEMBELEA OFISI ZA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

   


Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwasili katika Bandari  ya  Zanzibar alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi leo Septemba 26, 2016.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai akilakiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid, alipowasili katika Ofisi za Baraza hilo, leo. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mgeni Hassan Juma
 


Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid, alipowasili katika Ofisi za Baraza hilo, leo. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mgeni Hassan Juma
  


Spika wa Bunge Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo, Mgeni Hassan Juma.


Spika wa Bunge Job Ndugai kiwasalimia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alipotambulishwa wakati wa kikao cha Baraza hilo
 


Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mgeni Hassan Juma.Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zuberi Ali Maulid akimuelezea jambo Spika wa Bunge Job Ndugai wakati wa ziara hiyo. Picha na Ofisi ya Bunge
Post a Comment