Sunday, September 18, 2016

PPF yakabidhi mfano wa hundi katika matembezi ya hisani ya kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera


RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto), ambayo waliiahidi kwa Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuchangia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele.
RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi (wa tatu kushoto)  akiongoza matembezi ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na maeneo ya jirani. Wengine alioambatana nao ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maige, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi, Mbunge wa Jimbo la Muleba, Prof. Anna Tibaijuka pamoja na wengine wengi.
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki matembezi ya hisani ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo, kabla ya kuanza kwa matembezi ya hisani ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Mhe Balozi Mbelwa Kairuki katika viwanja vya Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay wakati wa shughuli ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na maeneo ya jirani.
Wananchi na Wadau mbalimbali wakifuatilia taarifa ya Maafa na shughuli ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na maeneo ya jirani

No comments: