Wednesday, September 14, 2016

KAMPENI YA DECLUTTER AND DONATE YAZINDULIWA DAR ES SALAAM

 Katikati - Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampeni ya Declutter and Donate Bi. Nasra Karl akiongea na waandishi wa habari katika mkutano jijini Dar es Salaam (kushoto) Hyacinta Ntuyeko - Mkurugenzi wa Glory Sanitary Pads (Kulia) Aunty Sadaka - Lifestyle Consultant na kushoto kabisa Bi Stella Malisha - Mkurugenzi wa IS Duke International.
 Aunty sadaka akitilia mkazo umuhimu wa kampeni ya declutter and donate kwa waTanzania wote. Kushoto kwake ni Bi. Stella Mashila Mkurugenzi wa IS Duke International.
 Bi Hyacinta Ntuyeko wa Glory Sanitary Pads akijibu swali kutoka mwandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Declutter and Donate iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Bi Nasra karl Mwanzilishi na Mkurugenzi ya kampeni ya Declutter and Donate na pembeni yake Aunty Sadaka Lifestyle consultant.
Bi Nasra Karl, Mkurugenzi na Mwanzilishi ya kampeni wa Declutter and Donate akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

KAMPUNI ya Elite Organizing Services Limited imezindua kampeni inayoitwa Declutter and Donate jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa kampeni ya aina hii kuzinduliwa nchini Tanzania. Kampeni ya Declutter & Donate ni mpango wa kijamii unaohamasisha umma kugawa vitu ambavyo hawavihitaji.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampeni Bi Nasra Karl alisema “wazo la kuanzisha kampeni hii lilikuja hapo mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli alivyotamka kuwa siku ya Uhuru itasherekewa kwa kufanya usafi ila kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.  Hapo basi tulikuja na wazo yakuanza kusaidia nyumba na biashara mbali mbali kuepukana na vitu wasiyo hitaji ambayo inasaidia kukuza mazingira safi na kusaidia kuzingatia ubora katika maisha yetu ya kila siku. 

Kuwa kampuni ya uandalizi inayotoa huduma kusaidia watu binafsi na biashara mbali mbali kuepuka kuishi na vitu wasiyo viihitaji na maisha ambayo yanampangilio, ELITE ORGANIZING SERVICES LIMITED iliona haja ya kuongeza uelewa kuelimisha umma maana ya kutoa vitu visivyo na umuhimu katika maisha yao ( declutter) na ni jinsi gani vinaweza kupunguzwa katika maisha ya watu na jinsi gani inaweza kutumika kwa manufaa ya wengine.  Kama msemo maarufu  ya kingereza inayosema ‘ Taka taka ya mwanaume moja ni dhahabu kwa mwanaume mwingine’ 
Kampeni ya Declutter & Donate Campaign itaanza mwezi wa tisa Septemba na kuisha mwezi wa kumi na mbili yaani miezi mitatu. 

Katika kipindi hiki tunawaomba watu binafsi, familia na biashara mbali mbali kugawa vitu vyao ambayo zimetumika na kuuuzwa katika yard sale, mwanzoni mwa Disemba tunategemea kuwa na tukio itakayo changisha kwa ajili ya kituo inayosaida watu. (charity).

Mwishoni mwa Disemba tutakuwa na tukio ambapo tutakuwa na wataalamu wa kudeclutter wakija kuongea na wa Tanzania na kuwaeleza jinsi ya kuepeukana na vitu visivyo na muhimu katika biashara zao, nyumba zao na maeneo yanayowazunguka.  

Mwaka huu kampeni ya Declutter & Donate watasaidia watoto yatima na wanawake wanaoishi katika mazingira magumu. Mwaka huu tunapenda kusaidia wanawake wanaopata shida katika usalama ya hedhi na  ‘Mtoto anayesoma atakuwa mtu anayeweza kufikiri’ kwa watoto wanao ishi katika mazingira magumu. 

Mara nyingi tukietembelea watoto yatima na kugawa chakula, nguo na vitu vingine vya kutumia kila siku tunasahau kwamba michezo na vitabu vina jukumu kubwa katika ukuaji bora wa motto na ndio maana tumeamua kuwapa michezo na vitabu.  


Tunapokea fenicha, vifaa vya nyumbani, vitabu vya watoto na michezo ya watoto. Hivi sasa tunaishughulikia mahala pakuacha hiv vitu na tutaweza kuwajulisha hivi karibuni kupitia vyombo vya habari.   
Post a Comment