Tuesday, September 20, 2016

MWENGE WA UHURU WAPITA KATIKA MIRADI 9 WILAYANI IKUNGI


Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe akimkabidhi Mwenge wa uhuru mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kulia).
Wananchi wakifatilia kwa karibu makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilayani manyoni kuhamia Wilayani Ikungi


Mkimbiza Mwenge Kitaifa Lucia vitalis Kamafa kutoka Manyara akiuhifadhi mwenge huo kwenye sehemu yake ya kuhifadhiwa



Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wa nne kutoka kushoto
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akisoma Maandishi yanayohimiza kuachana na Rushwa yaliyoandikwa na Klabu ya Rushwa Shule ya Sekondari Mkiwa 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Wilayani humo 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akiwasaidida kina mama kuwatwisha Ndoo kichwani mara baada ya kutembelea Mradi wa Maji wa Rafiki katika kijiji cha Muungano Kata ya Unyahati

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya stendi-Ikungi

Askari wakimbiza Mwenge wakiukinga Mwenge wa uhuru ili usizimike kutokana na upepo mkali unaovuma Wilayani ikungi, mkoani Singida
Usafiri unaotumika kuubeba Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida
Wananchi kwa umakini mkubwa wamejitokeza kushuhudia ujio wa Mwenge wa Uhuru
Viongozi mbalimbali wa serik;ali na chama cha Mapinduzi wakiulaki Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu akitoa ratiba ya kukimbiza Mwenge wa uhuru Wilayani humo 
Waandishi wa habari nao wapo na umakini mkubwa katika kuandika habari kuhusu Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe na mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakisalimiana baada ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru


Na Mathias Canal. Singida

Takribani Kilomita 141.5 zimetumika kukamilisha ziara ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Ikungi ambapo umepita kwenye Miradi tisa yenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni 975,991,180.44 kati ya miradi hiyo, Miradi mitatu imewekwa mawe ya msingi, Mradi mmoja umefunguliwa, Miradi mitano imezinduliwa, Miradi sita imekamilika sawa naasilimia 67 na miradi mitatu itakamilika ifikapo June 30, 2017.

Ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 umebeba ujumbe unaosema “Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa” na kauli mbiu isemayo “Washirikishwe na Kuwezeshwa” ukiwa umejikita katika kuhimiza dhana ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo, Usimamizi wa Miradi na pia kuunda Vikundi vitakavyo wawezesha kukopa na kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa George Jackson Mbijima amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ni tunu muhimu kwa Taifa na una lengo la kumulika mahali kulipokosekana matumaini, upendo na amani na hatimaye kurejeshwa sambamba na kumulika Miradi mbalimbali ya serikali na watu binafsi ili kuamsha ari ya utendaji uliotukuka na kurahisisha shughui za maendeleo katika jamii.

Amempongeza Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kubadilisha kasumba ya utendaji kazi wa mazoea kwa watumishiwa mbalimbali umma na taasisi za watu binafsi nakurejesha uwajibikaji kwa kila mmoja jambo ambalo limeamsha ari ya uwajibikaji kwa jamii na watanzania kwa ujumla.

Mbijima ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kwa kumbeza Rais kwa utendaji kazi wake jambo ambalo amesema kuwa jambo hilo littavifanya vyama hivyo kuzidi kupoteza mvuto kwani hiyo ni adhabu ya udanganyifu mwingi ambao viongozi wa vyamahivyo wamekuwa wakiufanya kwa kipindi kirefu katika mikutano yao.

Amesema kuwa watanzania wa sasa wanahitaji uwajibikaji, kukuza uchumi wa kila mmoja mmoja kwa kushirikiana na serikali hivyo uongo ukizidi bila mafanikio ya utendaji itakuwa sehemu ya kipimo cha kuwakataa wakati wa kuomba ridhaa tena baada ya miaka mitano ya uongozi wao.

Akisoma risala ya utii ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa Mbio za Mwenge wa uhuru Wilayani humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka alisema kuwa Ujumbe huo wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu kwa vijana unatilia mkazo kwamba maendeleo hayazuki yenyewe bali jamii kwa pamoja kuwa na kiu na ari ya kufanya kazi ili iweze kutumika katika kubuni, kupanga na kuweka mikakati inayotekelezeka na kutekeleza kwa maslahi mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia Hali ya Maambukizi ya UKIMWI Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa Mwaka 2015 jumla ya watu 8106 sawa na asilimia 56.6% walipima kwa hiari na jumla ya watu 288 (Wanaume 102 na wanawake 186) waligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI sawa na asilimia 3.5%,

Kwa mwaka 2016 Januari hadi June jumla ya watu 8158 (Wanaume 3657 na Wanawake 4501) walipima kwa hiari na jumlaya watu 301 (Wanaume 121 na wanawake 180 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU/UKIMWI sawa na asilimia 3.7% na hadi kufikia June 2016 jumla ya watu 2248 (Wanaume 651 na wanawake 1597) wamesajiliwa kwenye vituo vya Tiba na maangalizi CTC kwa ajili ya kupata dawa za kufubaza VVU nakati yao jumla watu 1749 sawa na asilimia 77.8% wameanzishwa kupata dawa za kufubazaVVU-ARV (Wanaume 591 na wanawake 1378 sawa na asilimia 86.3%.

Turuka amesema kuwa katika kupambana na VVU/UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi inaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi ili kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono kupitia mikutano ya hadhara, kutoa vipeperushi kwa njia ya mafunzo elekezi, ushauri wakitaalamu pamoja na kuonyesha Sinema/Video zinazoonyesha maambukiziya VVU na UKIMWI na jinsi ya kujikinga.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu amesema kuwa chini ya kauli mbiu “Tujenge jamii yenye afya bila dawa za kulevya” Wilaya yake inalaani vikali matumizi ya dawa za kulevya na unywaji pombe uliokithiri kwa kushirikianana wadau na wananchi wote kwa pamoja ili kuondokana na kadhia hiyo inayoathiri nguvu kaziya Taifa yaani vijana.

Dc Mtaturu alisema kuwa pia Wilaya hiyo kupitia taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Singida na wadau wake imeendelea kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara, vipeperushi na majarida, Semina na kuunda klabu za wapinga Rushwa mashuleni na sehemu za kazi ambapo mpaka sasa Wilaya ina klabu 20 za wapinga Rushwa.

No comments: