Wednesday, September 28, 2016

WAZIRI LUKUVI AWAFUTIA HATI WALIOMIKISHWA ENEO LOTE LA MAKABURI YA KINYEREZI SOKONI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja. 

Katika sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo mara moja ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu na Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na kufikishwa ofisini kwake kesho.

Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam, Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia kwa kuwachukulia hatua za kisheria.

Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
Waziri Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo
Waziri Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua
Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo
Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam, Leo Komba (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
" Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?" Sawa kuanzia mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la makaburi haya", alisema Waziri Lukuvi na kuongeza " Na wale waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja".
Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili.
Waziri Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kweneye eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson Celestine. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments: