Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma "Premier Club" pamoja na Kadi ya Kimataifa ya TemboCardVisa Infinite uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati wa uzinduzi wa TemboCard Visa Infinite pamoja na uzinduzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa cha Premier Club.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akipeana mkono na Dk. Kimei.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimkabidhi Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kadi ya kimataifa ya ‘TembocardVisa Infinite’, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo uliokwenda sambamba na kituo cha kutolea huduma ‘Premier Club’ jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi Kadi ya TemboCard Visa Infinite Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.
Naibu Spika Dk. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay (wa tatu kushoto).
Baadhi ya wageni waalikwa.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi huo.
Katibu wa Benki ya CRDB John Rugambwa akiwa katika uzindui huo.
Meza Kuu.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay.
Kutoka kushoto ni Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Mkuugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela wakicheza Kwaito wakati wa hafla hiyo.
NA ZAWADI CHOGOGWE
BENKI ya CRDB imezindua kituo cha kisasa kwa ajili ya kuhudumia wateja wakubwa kijulikanacho Premier Club katika jengo la Viva Tower.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei alisema Benki hiyo,imeamua kuzindua huduma hiyo pamoja na kadi maalum ya TemboCard Visa Infinite kwa ajili ya watejawa kundi hilo ikiwa ni mkakati wa Benki hiyo kuboresha huduma kwa wateja wa kundi hilo.
Kimei alisema lengo ni kuboresha huduma kwa wateja ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.
“ CRDB Bank Premier Club ni kituo maalum ambacho Benki hiyo imekizindua kwa ajili ya kuhudumia wateaja kundi hili maalum”alisema Dk.Kimei.
Dk. Kimei alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo, ya wateja maalum kitasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Benki kwa wateja huku akiamini huduma hiyo itakua ni chachu ya kuboresha huduma kwa wateja kwa Benki hiyo kwa ujumla.
Akiongelea juu ya huduma zitakazotolewa katika kituo hicho cha kisasa,Kimei wateja waliojiunga na huduma hiyo watapewa kadi maalum ijulikanayo TemboCard Visa Infinite huku wakipewa kipaumbele katika huduma mbalimbali pamoja na kupata nafuu ya tozo na riba katika huduma watakazo zitumia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya CRDB Tully Mwambapa, alisema kadi hiyo ni kadi ya kifahari zaidi na imetengenewa kwa teknolojia ya hali ya juu kuliko kadi zote za kimataifa za malipo duniani.
“Naomba kuzitaja baadhi ya tu ya huduma ambazo wateja wetu wataweza kupata kupitia huduma kupitia kadi hii ya TemboCardVisa Infinite watejawatapewa bima ya safari pamoja na familia zao endapo watafanya malipo kupitia kadi.”alisema Mwambapa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema, Benki ya CRDB ilikuwa ya kwanza kuingiza sokoni kadi ya malipo yaani "TemboCard" ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuwapa wateja uhuru wa kupata huduma kwa muda na mahali wanapotaka.
"TemboCard iliendelea kupata umaarufu zaidi pale ilipoongeza huduma ya kuweza kutumika nje ya nchi, au kupitia ATM za mabenki mengine, baada ya kuungana na makampuni makubwa yanayotoa huduma za kadi ya Visa, MasterCard na China Union na hivyo kuunda TemboCardVisa. TemboCard, MasterCard na hivi karibuni TemboCard China Union Pay" alisema Ndugu Laay.
Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB alisema Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB ina jukumu la kuweka mazingita bora ya uzalishaji yatakayosaidia menejimentina wafanyakazi kufikia malengo ya kibiashara huku wakiweka mahitaji ya wateja mbele zaidi.
" Bodi inathamini na kutoa kipaumbele utumiaji wa teknolojia na ubunifu wa wafanyakazi wake ili kuboresha na kurahisisha huduma zake kwa wateja na hii ndio nguzo ya pekee ambayo imeifikisha Benki yetu katika mafanikio haya makubwa ambapo leo hii tunazindua huduma hizi za "TemboCardVisa-Infinite" na kituo cha kisasa cha huduma kwa wateja wa Premier yaani "CRDB Bank Premier Club" alisema Ndugu Ally Laay.
Akiongea katika hafla hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuzindua huduma hizo za Premier Club na TemboCardVisa Infinite pamoja na mafanikio ambayo benki hiyo imeyapata na kuendelea kuyapata ambayo yana akisi sera ya serikali na adhma ya Bunge ya kutaka kujuimuisha wananchi wengi zaidi katika mfumo halali wa fedha.
"Mimi nikiwa kama kiongozi wa Bunge ambalo ni muhimili wa mkubwa wa nchi yet, nimekuwa nikifarijika sana kwa namna ambayo benki yetu ya CRDB imeendelea kukua na kuimarika na hivyo kuonyesha kuwa hata sisi watanzania wenyewe tunaweza "Tunawapongezeni na Hongereni sana" alisema Dk. Tulia.
Comments