WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) KWENYE MKUTANO WA ALAT MJINI MUSOMA


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhani akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika  mjini Musoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene kuhusu majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi alipotembe banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi na wadau mbalimbali nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiangalia vipeperushi na machapisho mbalimbali kwenye banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. Mbele yake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani wakati alipotembelea banda la maonesho la Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani(kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid M. Hamid (katikati) na Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjaka wakiwa kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)mjini Musoma.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (Kulia), akizungumza na Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile (mbele yake) kwenye banda la maonesho la Tume hiyo wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma .Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Afisa Habari Christina Njovu na Afisa Utumishi wa Tume Veronica Mollel.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kushoto), akimuelimisha mkazi wa Baruti mjini Musoma, Ismail Adudu alipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume Emmanuel Kawishe, Naibu Katibu wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw. Kailima Ramadhani (kushoto), akimuelimisha mkazi wa Baruti mjini Musoma, Ismail Adudu alipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma.
Afisa Utumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Veronica Mollel akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kowak ya Rorya mkoani Mara wakati walipotembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mjini Musoma. 
Picha na Aron Msigwa na Hussein Makame –NEC.

Comments