Friday, September 16, 2016

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA JENGO LAKE MKOANI DODOMA

Wahandisi wa Kampuni ya Norplan Tanzania wakiendelea na kazi ya upimaji wa udongo kwa ajili ya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika eneo itakapojengwa ofisi hiyo inayopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo la ofisi hiyo itakuwa na ghorofa 6 na inatarajiwa kukamilika mwaka 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akipewa  maelezo na Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea eneo litakapojengwa jengo la ofisi hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 

Picha zote na Emmanuel Ghula. 

……………….. 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma kwa kuanza kujenga jengo lake mkoani humo. 

Jengo hilo litakalokuwa nyuma ya Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema jengo la NBS lilipangwa kujengwa jijini Dar es Salaam lakini kutokana na agizo la Rais imebidi jengo hilo lijengwe mkoani Dodoma. 

“Kabla ya agizo la Mhe. Rais, jengo la NBS lilipangwa kujengwa Dar es Salaam na tayari maandalizi yalikuwa yameshafanyika lakini kutokana na agizo hilo imetupasa kujenga jengo letu hapa mkoani Dodoma,” amesema Dkt. Chuwa. 

Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo hilo amesema atahakikisha anafanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa. 

“Nimepewa siku 12 za kumaliza suala zima la upimaji wa udongo katika eneo hili na mpaka sasa hali ni nzuri na nina uhakika kuwa kampuni yangu itamaliza kazi hii ndani ya muda uliopangwa,” amesema Mhandisi huyo. 

Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu utaanza rasmi mwezi Novemba 30 mwaka huu na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
Post a Comment