Sunday, September 18, 2016

UVCCM WAISHAURI SERIKALI KUTUMIA JESHI LA JWTZ KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI NA KUTATHMINI PAMOJA NA KUGAWA MISAAADA KWA WAATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA


 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa vija Shaka Hamidu Shaka akichangia damu kwenye viwanja vya mashujaa Mkoani Kagera kwaajili ya majeruhi wa wahanga wa tetemeko la ardhi.
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamidu  Shaka akibadhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu kwaajili ya wa waathirika wa tetemeko la ardhi

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

UMOJA wa vijana wa chama cha CCM Taifa(UVCCM)wameishauri na kuiomba selikari kutumia jeshi la wananchi JWTZ  katika zoezi la kuhakiki na kutathimini pamoja na kugawa misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Shaka Hamidu Shaka alitoa ombi hilo kwa kamati ya maafa ya Mkoa ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salumu Kijuu alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa waathirika wa tetemeko kuwa hawatendewi haki na wale wanaopita kufanya tathimini kwenye nyumba zao zilizoathirika.

"Jeshi la wananchi hawana chama wala Dini hivyo hawezi kubagua mtu nina amini watatenda haki kwa kila mwananchi aliyeathirika na itasaidia kuondokana na migogoro ambayo inaweza kujitokeza kwa wale watakaokosa haki zao pia watafanya zoezi kwa wepesi na uharaka zaidi kuliko hali ilivyo sasa"alisema Shaka

Wakati huo huo umoja huo umekikabidhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu.

"Umoja wa UVCCM Taifa tunawapa pole sana wahanga wote wa tetemeko la ardhi,ila tunawaomba wanasiasa wasitumie tetemeko hili kama sehemu ya kutangaza siasa zao,hili ni janga za watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za vyama wala dini zao"alisema

Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salumu Kijuu alisema kuwa mambo ya ubaguzi kwa waathirika wa tetemeko ameshayakemea sana na anaendelea kuyakemea ndiyo maana ameelekeza misaada yote ipitie ofisini kwake ili iwafikie walengwa kwa utaratibu mahususi uliopangwa.

"Endapo mtu yeyote atabainika anafanya ubaguzi nitamchukulua hatua kali sababu bado misaada inahitajika sana"alisema Mkuu wa Mkoa

Post a Comment