TAASISI YA MKAPA YA KABIDHI NYUMBA 22 KWA MKOA WA PWANI


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mkapa , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarest Ndikilo , na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wakishiriki kukata utepe kuashiria kukabidhiwa rasmi nyumba hizo,kutoka Taasisi ya Mkapa kwa ajili ya madaktari. 

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ambaye ni mgeni rasmi katika halfa fupi ya kukabidhiwa nyumba, akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridiwani Kikwete wakingalia kwa nje moja ya nyumba zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa kwa ajili ya kukaa madaktari katika jimbo hilo,wakiwa na madaktari.  


Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Dr.Ellen Senkoro akimuongoza mgeni Rasmi Dkt Kikwete kwenda kufungua Nyumba hiyo 
Baadhi ya wananchi wa Chalinze wakishuhudia ufunguzi wa nyumba hizo za kuishi madaktari katika eneo lao.
Jana Tarehe 13 September 2016 Taasisi ya Benjamin Mkapa ilikabidhi nyumba 22 ilizojenga Mkoa wa Pwani kwa msaada wa Taasisi ya Dunia ya afya ya Marekani. Mradi huo ambao kila nyumba iligharibu Milioni 54 ulikabidhiwa jana kwenye sherehe fupi iliyofanyika Katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze katika kijiji cha Msoga ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete.Wilaya zilizofaidika na mradi huo ni Mafia ambayo imepata nyumba 10 , Chalinze 10 na Bagamoyo 2.

Comments