Wednesday, April 01, 2015

WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE WATAKIWA KUFUATA TARATIBU NA SHERIA KWA MUJIBU WA VIBALI NA LESENI ZAO

Na. Johary Kachwamba – MAELEZO, DODOMA
…………………………………………….
Serikali imewataka wamiliki wa kumbi za starehe , mabaa na nyumba binafsi kufuata taratibu na sheria zilizowekwa kwa mujibu wa vibali na leseni walizopewa na mamlaka husika
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juma Nkamia ametoa wito huo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mhe. Hilda Ngowi, Mbunge wa Viti Maalum aliyehoji mkakati wa Serikali katika kudhibiti usumbufu wa kumbi za starehe kwa wakazi jirani.
“ni jukumu pia la kila mwananchi kuchukua hatua kwa kutoa taarifa katika vyombo husika kuanzia ngazi ya Serikali za Mtaa, Kata, Polisi, Halmashauri za Wilaya, BASATA pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya” alisema Mhe. Nkamia
Wito wangu kwa wamiliki wa kumbi za starehe, mabaa a nyumba binafsi ni kuwakumbusha wafuate taratibu na sheria ziliowekwa kwa mujibu wa vibali na leseni walizopewa na mamlaka husika.
Mhe. Nkamia aliwataka wananchi kuendelea kutaoa taarifa kama kuna ukiukwaji wa upigaji miziki holela wakati wa mchana na usiku, utumiaji sauti zajuu wa yombo vya mawasiliano na vipaza sauti kwa baadhi ya maeneo ili kuondoa usumbufu juu ya vyombo  vya mawasiliano na vipaza sauti kwa baadhi ya maeneo ili kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa wananchi wanaohitaji kupumzika, kujisomea, wagonjwa, wazee na wanaohitaji kutafakari masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Naye Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira) Billman Mahenge alisema wizara yake imeandaa kanuni za kelele na mitetemo kwa ajili ya kudhibiti upigaji wa muziki kwenye maeneo ya wazi ikiwemo baa, kumbi za starehe na makanisani.
Alisema kanuni hizo ambazo zimekamilika na kuchapishwa zitazinduliwa Aprili 13, 2015 na watazikaidhi kwa Baraza la Hifadhi ya mazingira (NEMC) kwa ajili ya utekelezaji wa kanuni hizo.
Alisema baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya wakosaji ni kutozwa faini, kupelekwa mahakamani au kufungiwa au vyote kwa pamoja.

No comments: