Rais Obama akirejea nyumbani baada ya kutoka likizoni huko Haiwaii ambako alikuwapo kwa siku kadhaa sasa akiwa huko anasemekana alikuwa akifuatilia matukio muhimu ya nchini mwake.
Hivi karibuni aliagiza kuchukuliwa hatua za ziada za kiusalama katika usafiri wa ndege, baada ya mtu mmoja kujaribu kulipua ndege moja ya shirika la Marekani iliyokuwa inaelekea Detroit kutoka mjini Amsterdam.
Mtu huyo ambaye anasemekana ni raia wa Nigeria, alikuwa abiria ndani ya ndege hiyo, yenye chapa AIRBUS 330 iliyokuwa imewabeba abiria 278, alizidiwa nguvu na wenzake alipojaribu kuwasha fataki wakati ndege hiyo ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege huko Detroit.
Vyombo vya habari vya Marekani, viliripoti kuwa mtu huyo amewaambia maafisa wa usalama kuwa alitoa fataki hizo na maagizo ya kuilipua ndege hiyo kutoka nchini Yemen.
Comments