kamati ya bunge maendeleo ya jamii yatembelea chuo cha sanaa Bagamoyo leo


Mbunge wa Mbinga Magharibi Capt. John Komba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii akichangia mjadala kuhusu hali ya utamaduni nchini wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati hiyo katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana mchana. Picha na mdau Aaron Msigwa wa Maelezo.

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Juma Bakari akitoa ufafanuzi kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya maendeleo ya Jamii mara baada ya kuwasili jana mchana kuhusu mkakati unaoendelea wa kuiboresha Taasisi hiyo katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya elimu na Miundombinu. Kushoto ni mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Jenista Muhagama na Naibu waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera.

Comments