Tuesday, January 12, 2010

KAMATI NDOGO YA EALA YAKUTANA ARUSHA



Kamati ndogo ya uongozi ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) inakaa mjini
Arusha chini ya mwenyekiti wake Abdullah Mwinyi kujadili ripoti ya
mafanikio ya miaka miwili na nusu tangu kuapishwa kwa Bunge la Pili.

Mwinyi alisema kua baada ya kujadili taarifa hizo watapeleka mapendekezo
yao katika kikao cha Kamati kuu ya uongozi chini ya Spika wa Bunge hilo
kitakachokaa mwishoni mwa wiki hii.

Baadae kamatikuu hiyo itapeleka mapendekezo yake katika kikao cha tatu cha
bunge hilo kitakacho kaa kitika nchi ya Uganda, Kampala mwezi wa pili mwaka
huu.

Kamati hiyo inaundwa na Wajumbe kutoka nchi zote tano Kenya, Tanzania,
Uganda, Rwanda na Burundi ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Tanzania Yaibuka Kidedea kwenye Tuzo za Utalii Duniani

Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya kimataifa kama “Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari” katika Hafla ya Fainali za Worl...