Kilimo cha umwagiliaji


Wallahi jitihada kama hizi zingelisambaa Tanzania nzima kwa wakulima kutumia njia za kisasa kama hizi nina uhakika tungekuwa tumepiga hatua kali sana ya maendeleo bila shaka tungefanana na Malaysia na Indonesia lakini hebu nambie kilimo chetu kilivyo noma.

Comments

mloyi said…
Kuna watu wanathamini sana afya na maisha bora kwetu! Angalia huyu jamaa anachofanya, hangojei tuletewe mbogamboga toka brazil na afrika kusini, yeye anazalisha mwenyewe. Cha kusikitisha ni kwamba dola anazookoa kwenye matumizi yasiyolazima zinaundiwa matumizi mengine mabaya zaidi kwa uchumi wetu na maisha yetu kuwa bora.
Wakati umefika wa kusaidia watu kama hawa waendeleze kilimo chao ili warahisishe maisha yetu. hatuhitaji wawekezaji toka nje kama wanavyotamkwa bungeni, kwani hata hao huwahawaji na mitaji toka kwao bali hukopa kwa kutumia jina la Serikali ya Tanzania! tuwapatie vijana wetu uwezo wa kukopa pia ili waendeleze miundombinu ya mashamba yao.