Obama ashinda uteuzi wa kugombea urais





Seneta wa jimbo la Illinois nchini Marekani Barack Obama ametangazwa mshindi katika mchuano wa kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Demokratik uchaguzi ambao umepangwa kufanyika hapo mwezi wa Novemba mwaka huu.

Obama amejishindia wajumbe wengi wanaohitajika ili kuweza kupata idhini ya chama katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa awali wa kuwania uteuzi kwa tiketi ya chama katika mchuano mkali uliodumu kwa miezi mitano dhidi ya seneta wa jimbo la New York Hilary Clinton.

Licha ya kujipatia idadi mkubwa wa wajumbe Clinton amegoma kukubali kushindwa na Obama.

Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini New York amesema bado hakufanya uamuzi juu mustakbali wake wa kisiasa.

Uwezekano wa Obama kushinda urais wa Marekani kwa wengi unaonekana kuwa unaweza kuboresha uhusiano wa kigeni wa Marekani uliodhoofika kwa muda mrefu.

Comments