Wednesday, June 11, 2008

Cameroon ndani ya nyumba



Sam Eto'oo akiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuivaa Stars.

CAMEROON jana iliwasili nchini na kikosi chake kamili, huku nahodha wake Rigobert Song akisema: "Tunaihofia Tanzania.Alisema baada ya kuona mikanda ya mechi mbili wanajua kuwa wamekuja kucheza na timu nzuri na isiyotabirika".

Cameroon, ambayo ilikosa fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Ujerumani mwaka 2006 baada ya kutibuliwa na Misri katika mechi ya mwisho, imewasili nchini siku nne kabla ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayofanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Jumamosi.

"Kuja kwetu mapema ni sehemu ya mikakati yetu ya kupata matokeo mazuri kwenye kundi letu, ili tuwe na nafasi nzuri kwenye mashindano makubwa duniani," alisema beki huyo wa zamani wa Liverpool.

"Tumeiona Tanzania mapema, lakini haina tatizo kwetu kwa kuwa kikosi chetu pia kimeteuliwa kwa kuzingatia ukubwa wa mashindano."

Cameroon inaongoza Kundi la Kwanza la michuano ya awali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda mechi mbili za kwanza dhidi ya Cape Verde na Mauritius kwa matokeo sanjari ya mabao 2-0 na 3-0 na inataka kumaliza hatua hiyo bila ya kupoteza mchezo.

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAZEE WA MIKOA YOTE NCHINI, AFUNGUA UKURASA MPYA WA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

  Dodoma, Agosti 27, 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na wazee wa Mkoa wa Dodoma pam...