Monday, June 09, 2008

Ndege ya jeshi yaungua, sita wafariki dunia

Habari tulizo nazo hivi sasa zinasema kuwa watu wanane amefariki dunia katika ajali ya helikopta ya jeshi la ulinzi iliyokuwa njiani ikitokea Arusha kuelekea Dodoma.

inasemekana abiria wake ambao bado haijathibitishwa kuwa ni raia ama askari walikuwa wanatokea arusha kwenye mkutano wa sullivan.

inasemekana waliokufa ni abiria sita na marubani wawili wa helikopta hiyo. habari kutoka kikosi cha anga ama airwing Ukonga imethibitisha habari hiyo na tayari ndege imeenda eneo la tukio na kwamba taarifa kamili itatolewa baadaye.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari Makao Makuu ya Jeshi ilisema helkopita hiyo ya JWTZ yenye namba 9507 iliyokuwa inarejea Dar es Salaam, ilianguka saa 6.40 mchana katika eneo la Oljoro nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Taarifa hiyo ilitaja waliofariki katika ajali hiyo ni marubani wawili, mafundi ndege wawili na abiria wawili. Ndege hiyo ilikuwa kati ya ndege mbili zilizokuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi, wakati wa mkutano wa Sullivan.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...