MGOMBEA wa kiti cha urais kwa tiketi ya upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai ameamua kujitoa katika marudio ya uchaguzi yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii.
Akitangaza uamuzi huo mjini Harare jana, Tsvangirai alisema hakuna maana ya kushiriki katika uchaguzi ambao kuna uhakika kuwa hauwezi kuwa huru na wa haki ambao matokeo yake yako mikononi mwa Rais Robert Mugabe.
Tsvangirai alisema kwua yeye pamoja na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) kwa sasa wanaelekeza nguvu zao katika kuiomba jumuya ya kimataifa kuingia nchini humo kwa ajili ya kuwalinda raia wake.
Uamuzi huo uliotangazwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha Baraza Kuu la MDC jana ni hatua inayomaanisha kuwa kwa sasa ushindi ni wa bure kwa Rais Mugabe ambaye ataendelea kubaki madarakani. Habari zaidi hebu soma cheki BBC upate habari hii kwa kina.
Comments
Ms Bennett