Monday, June 16, 2008

Vipanya marufuku Dar


Hawa jamaa nuksi sana mmesikia hilo balaa yaani kiufupi ni kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (Sumatra), imesema daladala aina ya Hiace, maarufu kama "Vipanya", hazitaruhusiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam, ifikapo Agosti Mosi, mwaka huu.

Badala yake, Sumatra imesema huduma hiyo itatolewa na magari makubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 25, badala ya "Vipanya", ambavyo vina uwezo wa kuchukua abiria 18 tu walioketi.

Hata hivyo, Sumatra imesema magari yatakayoruhusiwa kutoa huduma hiyo, lazima yawe ni mapya na yasiwe yametumika zaidi ya miaka mitano, kama inavyofanyika hivi sasa. Mpango huu bila shaka utafanya jiji la Dar es Salaam lisikalike kwa kuwa na vibaka..

Mkurugezi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa alisema uamuzi huo unatokana na kanuni mpya za viwango vya magari ya usafiri wa umma ambayo inazuia magari yenye uwezo wa kuketisha abiria chini ya 25 kutoa huduma za usafiri huo mijini.

Sekirasa alisema hayo kwenye mkutano wa wadau wa kukusanya maoni, kuhusu maombi ya wamiliki wa mabasi ya kuongeza gharama za usafiri Dar es Salaam, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini.

"Kwa mujibu wa kanuni mpya za viwango vya magari ya usafiri wa umma, magari yenye uwezo wa kuketisha abiria chini ya 25 hayafai kutoa huduma za usafiri wa umma," alisema Sekirasa. Habari zaidi hebu soma cheki Mwananchi upate habari hii kwa kina

No comments: