Mufti arejea nchini kinyemela



UJIO wa Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba, aliyetarajiwa kuwasili nchini akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari, moyo na mguu, jana uligeuka kitendawili.

Hali hiyo ilidhihirika baada ya waandishi na wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kumsubiri kwa zaidi ya saa sita katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam (IJNA), bila mafanikio.

Mbali na hilo, pia hakuna kiongozi, afisa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wala muumini yeyote wa Kiislamu, aliyekwenda uwanjani hapo kwa ajili kumpokea kiongozi huyo wa Waislamu nchini.

Taarifa za kurejea nchini kwa Mufti Simba (71), zilianza kupatikana saa 5:00 asubuhi jana, baada ya baadhi ya viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya Bakwata, kuwaarifu baadhi ya waandishi wa habari suala hilo. Soma zaidi www.mwananchi.co.tz katika habari iliyoandikwa na Na Muhibu Said.

Comments