Amanda wetu yuko juu miss Universe


Miss Universe Tanzania, Amanda Ole Sulul ameingia kwenye 20 bora kati ya warembo 80 wanaowania taji la mashindano hayo yanayoatarajia kufanyika Vietnam Julai 14.
Amanda ameingia hatua hiyo pamoja na mrembo wa Afrika Kusini, Tansey Coetzee ambapo warembo wa Misri, Ghana, Mauritius na Nigeria hawapo katika orodha hiyo.
Miss universe Venezuela Diana Mendoza anashika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo akifuatiwa na mrembo wa Marekani, Puerto Rico, Panama, Trinidad and Tobago, Mexico, Ireland, Australia, Colombia, na Thailand.
Pia wapo India, Monteneegro, China, Kosovo, Belgium, Japan, Curacao, Tanzania, Afrika Kusini na Italia.
Amanda ambaye alishinda taji la Miss Universe Tanzania Mei 29 mwaka huu, alitayarishwa na wataalam mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa kampuni ya Compass Communications.

Comments