Sunday, June 01, 2008

Sumaye akwepa ufisadi

Frederick Sumaye, aliyekua Waziri Mkuu wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa
miaka kumi, leo amemtolea uvivu bosi wake wa zamani, Ben Mkapa kwa kukataa
kumtetea "kwa mambo binafsi" akisema kama ni utendaji wa serikali, anaamini
kia mtu anajua serikali ya awamu ya tatu ilifanya kazi nzuri, lakini wapo
watu binafsi mmoja mmoja waliofanya makosa na kwa kuwa wanachunguzwa
watahukumiwa kwa makosa yao na si serikali nzima....

Akatoa mfano wa ununuzi wa rada, ujenzi wa barabara, ununuzi wa ndege, uwekezaji na mengineyo kuwa ni mambo ambayo yana manufaa kwa taifa, lakini kupitia maamuzi hayo mema wako watu ambao walifanya uhalifu kama vile kula rushwa na kuhujumu uchumi
watu ambao alisema wanastahili kuhukumiwa kwa makosa yao binafsi baada ya
kuchunguzwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Alipoulizwa kwanini hamtetei Mkapa alisema, "Kama angekua anatuhumiwa kama
kiongozi wangu ningemsaidia kujibu, lakini jamani mambo binafsi mimi siwezi
kumsemea, Kwani mimi ni mtoto wake?... Si alisema kule Lupaso? Naona
hakumridhika,mbona hata Bush anaweza kwenda katika ranchi yake
kuzungumzia mambo?"

Akasema yeye anajiamini kuwa ni safi mbali ya kuwapo maneno machafu dhidi
yake, akirejea sababu ya kuzungumza na waandishi leo, ambako alikua mualikwa
katika mkutano wa uongozi wa gazeti la Tanzania LEO (Limekufa) ambao ulifika
kumuomba radhi kwa habari yao ya kwamba ana trilioni kumi nje ya nchi na
akaunti zake zimezuiwa na JK.
cheki
MWANAHABARI ANAVYOSEMA

No comments: