Friday, March 28, 2008

CCM mambo mazito butiama







Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara.

Kikao hicho kimeanza tu muda siyo mrefu baada ya Rais Kikwete kuwa amewasili Butiama tayari kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM .

Kikao cha NEC kinaanza kesho ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika kijiji ambako alizaliwa Baba wa Taifa na mwanzalishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Kikwete aliwasili Butiama kwa barabara akitokea Mwanza ambako ndege yake ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza mapema asubuhi na akaamua kusafiri kwa gari kwenye Musoma.

Mjini Mwanza, mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake, walijitokeza kwa wingi, katika baadhi ya sehemu za jiji hilo mvua ikiwa inanyesha, kumshangilia Rais wakati msafara wake ukikatisha mitaa ya jiji hilo kuelekea Musoma.

2 comments:

Anonymous said...

MZEEE MBONA PICHA HAZIONEKANI..NA HUKO DODOMA WANATAMBIKA NINI, TUNATAKA KILA KITU KIENDE KWA UWAAZI NA UKWELII.. MAAANA TUMESHAZIKIA KWAMBA TUMESIMAMISHIWA MISAAADA KUTOKA KWA MATAJIRI...

Anonymous said...

hivi huk chamwino kuna lipi jipya