Tuesday, June 07, 2016

VANESSA MDEE ATEMBELEA TTB NA KUAHIDI KUSHIRIKIANA NAYO KATIKA KUTANGAZA UTALII

Vanessa Mdee Mdee (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB (kushoto), Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza na Meneja Masoko wa TTB  Bw. Geofrey Meena.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi (kulia) akijadliana jambo na Vanessa Mdee  leo walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania.

Mwanamuziki maarufu wa Bongo fleva nchini Tanzania Vanessa Mdee amesema yuko tayari kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kuvitangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani nab nje ya nchi.
Mdee ametoa ahadi hiyo alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii leo jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo na uongozi wa Bodi hiyo kuhusu namna TTB inavyoweza kushirikiana nae katika kutangaza na utalii wa Tanzania.

Ujio huo wa mwanamziki huyo ambaye pia ni nguli wa miondoko ya R&B, Hip Hop, na Afro Pop ulifuatia mwaliko wa uongozi wa TTB kuomba kukutana na kuzungumza na mwanamuziki huyo katika azma na mkakati wa TTB kuwatumia wasanii na watu wengine maarufu nchini katika kutangaza Utalii wa Tanzania.

Katika mazungumzo hayo Vanessa Mdee amesema yuko tayari kufanya kazi na TTB kwa lengo la kutangaza vivutio vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwa balozi wa hiari wa Utalii “ Tutaendelea kujadiliana kuona ni namna gani nzuri tunaweza kushirikiana, na mimi niko tayari kuifanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa hiari wa Utalii” alisema Mdee.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi alielezea kufurahishwa kweke na utayari wa Vanessa Mdee katika kuunga mkono juhudi za TTB katika kuutangaza na kuundeleza Utalii wa ndani sambamba na ule wa Kimataifa, na kuahidi kukamilisha haraka mchakato mazungumzo hayo na hatimaye kusainiwa kwa makubaliano baina ya pande hizo mbili.

Katika kutekeleza jukumu lake la kuitangaza vivutio vya Utalii Tanzania ndani na nje ya nchi Bodi ya Utalii Tanzania imekuwa ikibuni na kutekeleza mbinu na mikakati mbalimbali kama vile kuweka matangazo katika televisheni za kimataifa, kutumia mitandao ya kijamii viwanja vya mipira ya miguu, kuandaa safari za waandishi wa habari, kutumia watu maarufu na njia nyinginezo nyingi.
Post a Comment