Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 24 Februari 2026 aliwasili katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo mkoani Dodoma kwa ziara rasmi ya kikazi.
Akiwa katika makao hayo ya kimkakati, Rais alipokelewa na viongozi waandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na maafisa wa ulinzi na usalama. Ziara hiyo imelenga kukagua shughuli za kiulinzi, kupokea taarifa ya hali ya usalama wa nchi na kuimarisha utendaji wa vyombo vya ulinzi.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais alisisitiza nidhamu, uzalendo na weledi katika kulinda mipaka ya nchi, rasilimali za Taifa na usalama wa wananchi, akiahidi kuwa Serikali itaendelea kuimarisha maslahi na vitendea kazi vya wanajeshi ili kuongeza ufanisi.
Ziara hiyo imeonesha dhamira ya dhati ya Amiri Jeshi Mkuu katika kusimamia kwa karibu masuala ya ulinzi na usalama wa Taifa.
#RaisSamia
#AmiriJeshiMkuu
#UlinziWaTaifa
#MMUTKikombo
#Dodoma
#Tanzania

.jpeg)





No comments:
Post a Comment