Wednesday, May 06, 2015

RITA YAENDELEA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANAFUNZI WILAYA YA KINONDONI

01
Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani} jana Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya kampeni ya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi za Manispaa ya Kinondoni ambapo amesema hadi sasa zaidi ya wanafunzi Elfu 5 wamesajiliwa na kupata vyeti. Kulia ni Msajili wa Vizazi na Vifo Wilaya ya Kinondoni Bi. Mariam Ling’ande.
02
Msajili wa Vizazi na Vifo Wilaya ya Kinondoni kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi. Mariam Ling’ande akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani} jana Jijini Dar es Salaam kuhusu taratibu za kufuata ili kupata cheti cha kuzaliwa na kutoa rai kwa wananchi kuacha kutumia vishoka ambao hutoa vyeti bandia badala yake wafike kwenye ofisi za RITA zilizopo kote nchini. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Josephat Kimaro.
03
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA FATMA SALUM – MAELEZO

No comments: