Sunday, May 17, 2015

BENARD MEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA QASWIDA


indexNa Mwandishi  Wetu
……………………………..
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Qaswida lililoandaliwa na Ulamaa Promotions Centre litakalofanyika  Mei 24 kwenye viwanja vya sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, ustadh Jumanne Ligopora
Ligopora alisema wamejipanga katika tamasha hilo kushirikisha madrasa zaidi ya 50 za jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa.
Aidha Ligopora alisema hivi sasa wako kwenye mchakato wa kusambaza mialiko kwa madrasa za Dar es Salaama na mikoani.
“Tunatarajia maelfu ya Waislamu kumiminika kwa wingi katika viwanja vya Benjamin Mkapa kwa lengo la kupata ladha mbalimbali za Qaswida,” alisema Ligopora,” alisema Ligopora.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya maandalizi, alisema wameshapeleka taarifa kwa madrasa mbalimbali za jijini Dar es Salaam  na nyingine zilizoko mikoa jirani.

No comments:

MMUYA: WANANCHI WANUFAIKE NA UWEKEZAJI WA NHC KUPITIA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maghala unaotekelezwa na S...