Wednesday, April 08, 2015

MWAKILISHI MKAZI WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI, AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), wakati kiongozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke, anayefuata ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, Joyce Mends-Cole.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania.  Rodriguez alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

TANZANIA INA FURSA KUBWA YA KUENDELEZA NISHATI YA JOTOARDHI; WAZIRI NDEJEMBI ALIELEZA BARAZA LA IRENA

📌Asisitiza ushirikiano wa taasisi za kifedha na Jumuiya za Kimataifa hasa katika hatua za utafiti 📌Akaribisha wawekezaji; Asema Serikali i...