WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WA KITUO CHA CHILD IN THE SUN WAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE NA TCAA
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwilaakimkabidhimsaada wa Madaftari na vyakula mbalimbali Samson Ali (12) ambaye ni mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu ambao hivi sasa wanalelewa katika Kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki.watoto hao wanapatikana kwa kukusanywa mitaani. Mwalimuwa Kituo cha Kulea watoto waishio katika mazingira Magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, Martin Modest akipokea Msaada wa Vyakula na Vifaa vya Shule yakiwemo Madaftari kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila ,Watoto hao wanapatika kwa kukusanywa kutoka mitaani na kulelewa hapoambapo wanapatiwa ushauri kabla ya kuanzishwa shule. Watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleya watoto waishio katika mazingira magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, wakifurahia madaftari waliyokabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwilaambaye ndiye aliyekabidhi msaada huo. Watoto wanaoishi katika Mazingira magumuambao wanalelewa katika kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, kikiwa chini ya Kanisa Katolikiwakibeba mizigo ya vyakula mbalimbali na vifaa vya shule baada ya kukabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd.
No comments:
Post a Comment