Saturday, July 12, 2014

Jopo la Wahariri latembelea miradi ya nyumba za gharama nafuu wa NHC Mtanda, Lindi na Shangani Mtwara

Juzi, Alhamisi (Julai 10, 2014) na jana Ijumaa (Julai 11, 2014) jopo la Jukwaa la wahariri takriban 85 walitembelea kwenye miradi yetu miwili, mmoja wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda mkoani Lindi na mwingine wa nyumba za makazi za kati na juu zilizopo eneo la Shangani Mtwara.
Jopo hilo likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda na Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena. Walisomewa taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Nyumba hizo zipatazo 30 Lindi ambazo sasa zimefikia kwenye hatua za mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa wamiliki wake kwani nyumba zote 30 tayari zilishanunuliwa na zile za Mtwara ambazo pia ni 30, 10 kati ya hizo zikiwa zimeshanunuliwa.
Miongoni mwa mambo makubwa yaliyozungumzwa na wahariri hao ni kuliomba kuendelea kusimamia azam yake ya kuwauzia nyumba Watanzania wa kipato cha chini, kwani kwa kufanya hivyo watanzania wa kawaida watakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba na siyo kuendelea kuwa wapangaji wa shirika.



Meneja wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John akizungumza na wahariri walipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Shangani Mjini Mtwara leo jioni. Kutoka Kulia ni Theophi Makunga, Mhariri na Meneja Bishara wa Mwananchi Communications Limited, Jesse Kwayu Mhariri Mtendaji wa Nipashe na Bakari Machumu Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited. 


Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.

Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.


Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Meneja wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John walipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Shangani Mjini Mtwara leo jioni. Kutoka kulia ni Jabir Idrisa, Mhariri wa Mwanahalisi, Salim Salim nguli wa Habari na Mwalimu kutoka Zanzibar, Joseph Kulangwa wa Uhuru Publications.


Mojawapo ya majengo ya majengo ya Mradi wa nyumba za makazi za Shangani kama linavyoonekana leo hii. Ni mojawapo kati ya majengo matatu yenye nyumba 10 kila moja na hivyo kufanya idadi kufikia 30.


Meneja wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John akiwa  pamoja na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa , Yahya Charahani kwenye MRadi wa Shangani

Jopo la Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri (TEF) wakibadilishana mawazo muda mfupi baada ya kuwasili kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu wa Mtanda uliopo eneo la NHC Mtanda Lindi, Wahariri hao walifanya ziara ya kujionea utekelezaji wa mradi huo ambao unajenga sambamba na mingine 15 nchini na kupata taarifa fupi ya utekelezaji wake, wapo mkoani Mtwara katika mkutano wao wa kawaida kutafakari masuala mbalimbali katika sekta ya habari.  
Jopo la Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri (TEF) wakitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu wa Mtanda uliopo eneo la NHC Mtanda Lindi, Wahariri hao walifanya ziara ya kujionea utekelezaji wa mradi huo ambao unajenga sambamba na mingine 15 nchini na kupata taarifa fupi ya utekelezaji wake, wapo mkoani Mtwara katika mkutano wao wa kawaida kutafakari masuala mbalimbali katika sekta ya habari.  
 Nyumba za mradi wa nyumba za gharama nafuu wa Mtanda Lindi zinavyoonekana.
 Meneja wa mkoa wa Lindi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mussa Patrick Kamendu akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Wahariri wakiwasili kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu wa Mtanda uliopo eneo la NHC Mtanda Lindi, Wahariri hao walifanya ziara ya kujionea utekelezaji wa mradi huo ambao unajenga sambamba na mingine 15 nchini na kupata taarifa fupi ya utekelezaji wake, wapo mkoani Mtwara katika mkutano wao wa kawaida kutafakari masuala mbalimbali katika sekta ya habari.  

Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Lindi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mussa Patrick Kamendu (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Nyumba za mradi wa gharama nafuu wa Mtanda Lindi zinavyoonekana.

No comments: