Wednesday, July 09, 2014

AIRTEL YAMWAGIA WAHARIRI VIFAA VYA MICHEZO

Meneja Uhusiano wa  Airtel, Jackson Mmbando,akiongea na waandishi wa habari  wakati wa   kukabidhi  vifaa vya michezo kwa Jukwaa la wahariri  kwaajili ya  mechi kati yao na timu ya waandishi wa mkoa wa Mtwara itakayofanyika ijumaa  tarehe 11 Julai mkoani Mtwara. Pichani ni  Nahodha wa timu ya wahariri Bwana Kulwa Karedia.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabithi Nahodha wa timu ya wahariri  Bwana Kulwa Karedia…
Meneja Uhusiano wa  Airtel, Jackson Mmbando,akiongea na waandishi wa habari  wakati wa   kukabidhi  vifaa vya michezo kwa Jukwaa la wahariri  kwaajili ya  mechi kati yao na timu ya waandishi wa mkoa wa Mtwara itakayofanyika ijumaa  tarehe 11 Julai mkoani Mtwara. Pichani ni  Nahodha wa timu ya wahariri Bwana Kulwa Karedia.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabithi Nahodha wa timu ya wahariri  Bwana Kulwa Karedia ,  vifaa vya michezo kwaajili ya mechi kati ya timu ya Jukwaa la wahariri na timu ya waandishi wa mkoa wa Mtwara itakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 11 Julai mkoani Mtwara
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh milioni 1.1 kwa timu ya Jukwaa la  Wahariri Tanzania (TEF).Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema uamuzi wa kutoa msaada huo umefikiwa kutokana na kutambua mchango wa vyombo vya Habari nchini.
“Tunafaurahi kuwaambia kwamba leo (jana),tunakabidhi msaada wa vifaa vya michezo ndugu zetu wahariri ambao wanajiandaa na mchezo wa kirafiki mkoani Mtwara Jumamosi hii.
“Kama kwa vile wahariri ni watu ambao wanakuwa na majukumu mengi ya kila siku kwenye vyumba vya Habari, tunaamini baada ya mkutano wao, watapata fursa ya kucheza mchezo wa soka pale Mtwara ili kuweka miili yao sawa,”alisema Mmbando.Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na jezi seti moja,mipira mitano, filimbi tatu,fulana na traksuti tano.
“Hii ni sehemu tu ya msaada mdogo,tunategemea vitawasaidia jamaa zetu kuonyesha makekeo yao,”alisema Mmbando.Akipokea msaada huo, Nahodha wa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Kulwa Karedia aliishukuru Airtel kwa msaada huo na kusema umekuja wakati mzuri.
“Unajua mawasiliano bila waandishi wa habari hayapo, nadhani ndiyo maana Airtel wameona umuhimu wa kutoa msaada huu na sisi tunasema hatutawaangusha,”alisema Karedia.Alisema timu yake inatarajia kuondoka kesho kuelekea Mtwara ambako Jumamosi hii watacheza na timu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara.
Kikosi  cha TEF kinaundwa na wachezaji kama Theopil Makunga,Revocatus Makaranga,Jesse Kwayu,Manyerere Jackton,Ansbert Ngurumo,Salehe Mohamed,Neville Meena,Mnaku Mbani,Salim Said Salim, Wallace Maugo na Erick Anthony ‘Chinga’.

No comments: