Tuesday, July 08, 2014

UMATI NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA MAONYESHO YA 38 SABASABA

1
Lulu Ng’wanakilala Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishuglisha na elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa TANTRADE katika viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam jana, Mkurugenzi huyo amesema UMATI inalo jukwaa la vijana linalokutano kila mwezi kwa ajili ya vijana kujaili mambo mbalimbali kuhusu afya ya uzazi kwa vijana na upimaji wa virusi vya ukimwi kwani afya bora na mpangilio wa uzazi ndiyo maendeleo ya kijana, ukipanga uzazi na mipango ya maendeleo inakwenda vizuri, aliyeshika kipaza sauti ni Meshack molel Meneja Utetezi UMATI.
2
Ofisa Mawasiliano wa UMATI Bi Easter Mwanjesa akielezea jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya mkurugenzi huyo kuzungumza na wanahabari hao.
3
Bi. Zelda Mongi Mkufunzi kituo cha vijana UMATI Temeke akiwahudumia wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda la UMATI ili kupata maelezo juu ya hudua za shirika hilo.
4
Baadhi ya maofisa wa UMATI wakiwa tayari kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wananchi wanaotembelea banda hilo.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...