Saturday, July 26, 2014

ASKOFU MKUU WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM MUADHAMA POLYCARP KARDINALI PENGO AWAPONGEZA WALIOFANYA VIZURI MITIHANI YA KIDATO CHA SITA 2014 KUTOKA SHULE YA SEKONDARI YA ST JOSEPH YA JIJINI DAR ES SALAAM


 Kufuatia kufanya vizuri kwa Shule ya Sekondari ya St. Joseph ya Jijini Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo Julai 18, mwaka huu alikutana na wanafunzi wa tatu walioongoza Kitaifa na kuongoza kwa masomo na kuwapa pongezi.



Pichani juu ni Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, akisalimiana na wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa kutoka shule ya Sekondari ya  St. Joseph Cathedral ya Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki ambao ni , Joseph Ngobya wa masomo ya Sanaa na Lugha, Isaack Shayo aliyeshika namba moja kitaifa (katikati) na Prince Mwambaja (wapili kushoto) aliyeshika nafasi ya tano kitaifa masomo ya biashara.
  Wazazi walimpa Kardinali zawadi kwa kuanzisha shule hiyo na kutoa elimu kwa vijana wao.
  Mwalimu Mkuu,Sr. Theodora Faustine akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Wanafunzi wakiwa katika Mkutano huo wa shukrani kwa Kardinali Pengo.
  Sr. Theodora Faustine ambaye ndio Mkuu wa shule ya Sekondari ya  St. Joseph Cathedral akizungumza.
read more

No comments:

*KAMISHNA KUJI AKAGUA ENEO LA KOGATENDE SERENGETI ASISITIZA MAAFISA NA ASKARI UHIFADHI KUENDELEA KUSIMAMIA SHERIA ZA HIFADHI ILI KUIMARISHA SHUGHULI ZA UTALII

Na. Philipo Hassan - Serengeti Kamishna wa Uhifadhi, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) CPA Musa Nassoro Kuji, leo Julai 24, 2025...