Thursday, July 10, 2014

Tanzania na Algeria zinakamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya Ubia itakayohusika na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na Kampuni ya Ubia ya kujenga mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas” (LPG) na kuiuza gesi kwa wananchi kwa kutumia mitungi.

 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Muhongo Wa kwanza kulia), akiongea jambo na wataalamu wa masuala ya gesi na umeme wa Algeria wakati walipokwenda kutembelea Mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa HAMMA ,Mtambo huo wenye uwezo wa kuzalisha mewagati za umeme 418 unamilikiwa na Serikali ya Algeria kwa asilimia 100.
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuanzisha kampuni za Ubia za ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na ujenzi wa Mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas’ (LPG) ambayo itauzwa kwa wananchi kwa kutumia mitungi. Walio upande wa kulia ni Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi, Algeria (wanne kutoka kulia) na ujumbe wake.

No comments: