Wednesday, July 09, 2014

MAGUFULI AZINDUA KIVUKO KIPYA BUNDA

Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara. “Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema Waziri Magufuli Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.

Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.

Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.

“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli. Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.

Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA NA MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA VIJIJINI.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO ALIYESSIMAMA KULIA NA MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA WAKWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPUNGIA WAKAZI WA MWIBARA MARA BAADA YA KUFUNGUA KIVUKO CHA MV MARA.
WADAU WAKIFATILIA TUKIO HILO
PICHA YA BOTI AMBAYO ILIKUWA IKITUMIKA AWALI KUVUSHA WATU KATI YA MAJITA NA IRAMBA KWA GHARAMA YA SHILINGI 2000/=.
 KIVUKO CHA MV MARA
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPOKEA ZAWADI ZA KIMILA KUTOKA KWA WENYEJI WA BUNDA ZA KUMTAMBUA KUWA MKAZI WA MJI HUO KWA KIMILA.
WAZIRI WA UJENZI MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA WAKAZI WA IRAMBA KATIKA JIMBO LA MWIBARA KABLA YA KUZINDUA KIVUKO CHA MV. MARA CHENYE UWEZO WA KUBEBA TANI 25 YANI MAGARI MANNE NA ABIRIA 50.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIFURAHIA NA WANACHAMA WAPYA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WALIOAMUA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO MARA BAADA YA WAZIRI MAGUFULI KUMALIZA KUHUTUBIA MKUTANO.

No comments: