Monday, July 21, 2014

BALOZI WA PALESTINA AWAOMBA WANAHABARI TANZANIA KUPAZA SAUTI

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo.
Sheikh Jalala (katikati) akizungumza katika mkutano huo.
Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Meza kuu ikifuatilia majadiliano katika mkutano huo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.
Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.
Baadhi ya wahariri na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na ubalozi wa Palestina.
BALOZI wa Palestina nchini Tanzania, Nasri Abu Jaish amevitaka vyombo vya habari nchini Tanzania kusaidia kupaza sauti dhidi ya vitendo vya uonevu na mauaji yanayofanywa kwa raia wa Palestina na taifa la Israel ili vitendo hivyo vikomeshwe mara moja.
Balozi Abu Jaish ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokutana na ubalozi huo kuzungumzia hali halisi ya mgogoro wa Palestina na taifa la Israel unaoendelea hadi sasa.
“…Mi naomba waandishi wa habari Tanzania andikeni ukweli juu ya uonevu huu wanaofanyiwa raia wasio na hatia, sitaki muandike kwa kupotosha semeni ukweli ili umma ujue nini kinachoendelea kwa Wapalestina ndani ya taifa lao…,” alisema Balozi Abu Jaish akizungumza na wahariri hao.
Pamoja na hayo Balozi Abu Jaish aliiomba Tanzania na mataifa mengine yanayopenda amani kuungana kwa pamoja na kupaza sauti kukemea uonevu wanaofanyiwa raia wa Palestina ndani ya ardhi yao, kwani sauti za wengi zinaweza kukomesha hali hiyo na hatimaye mauaji kwa raia wasio na hatia kukoma mara moja.
Aidha alisema kitendo cha taasisi za kimataifa kukaa kimya huku raia wasiokuwa na hatia wakionewa na wengine kupoteza maisha ni sawa na kubariki vitendo hivyo viendelee. “…Makosa yanayofanywa na taifa la Israel yanaweza kuwa ya ulimwengu mzima endapo tutaendelea kukaa kimya huku watu wakionewa na kuuwawa nchini mwao…kama kweli hatupendi haya yaendelee kwanini tunakaa kimya,” alihoji Balozi Abu Jaish.
Awali akiwasilisha mada kwa wahariri Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdul Sheriff alisema mgogoro wa Palestina na Israel unachochewa na ukandamizaji ulioanza kufanywa katika mgawanyo wa ardhi ya mataifa hayo tangu mwaka 1947.
Alisema chanzo cha Tatizo la Palestina lilianza tangu mgawanyo wa ardhi kati ya Wayahudi na Waarabu; katika mgawanyo huo waarabu ambao walikuwa wengi walipewa sehemu ndogo ya ardhi huku Wayahudi ambao walikuwa ni wachache walipewa sehemu kubwa ya ardhi.
Alisema mpango wa Mgao wa Palestina uliofanywa na Umoja wa Mataifa, UN mwaka 1947 uligawa nchi ya
Warabu milioni 1.2 walipewa ardhi kwa asilimia 43, huku idadi ya Wayahudi milioni 0.6 wakipewa ardhi asilimia 56 mgao ambao haukuwa sawa kimtizamo.
“…Israel ilipoiteka ardhi ya Kiarabu, pamoja na Palestina mwaka 1967, Baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere alikemeasema; “The establishment of the state of Israel was an act of aggression against the Arab people…Israel must evacuate the areas … – without exception- …we cannot condone aggression on any pretext, nor accept victory in war as a justification for the exploitation of other lands, or government over other peoples.“Huu ndio uliokuwa msimamo wa TZ 1967. Tulivunja uhusiano na Israel, na tulikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuipokea ubalozi wa Palestina.” Alisema Pref. Sheriff akihoji ukimya wa sasa.
Waandaaji wa mkutano huo pia walitangaza kufanya maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Quds Duniani yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2014; kwa Tanzania maandamano yataanzia Ilala Boma jijini Dar es Salaam kwenda Uwanja wa Kigogo na baadaye Karimjee ambapo kutakuwa na mada anuai.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments: