Wednesday, July 16, 2014

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI DK. CHARLES TIZEBA AONGEA NA WAFANYAKAZI WA WAKALA WA NDEGE ZA SERIKALI TANZANIA (TGFA)

DSC_0692
Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi katika Wakala wa Ndege za Serikali Tanzania (TGFA), Mhandisi Julius Shaba, akieleza jambo katika hanga ya Wakala huo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka kwa kulia), wakati alipotembelea ofisi za Wakala huo na kuongea na wafanyakazi hivi karibuni. Kulia wa Waziri Tizeba ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo Kapteni Kenan Mhaiki.
DSC_0696
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akifafanua jambo wakati akiongea na Menejimenti na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali Tanzania (Tgfa), alipokutana nao hivi karibuni. Naibu Waziri Tizeba aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuwahudumia vyema Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments:

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ashuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Ushirikiano Kati ya Tanzania na Angola

Luanda, Angola – 08 Aprili 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , leo ameshuhudia utiaji saini wa mi...