Thursday, July 10, 2014

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Filipe Nyusi alipowasili Jana jioni Julai 9, 2014, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
  Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
   Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana
   Nyusi akidhihirisha furaha kwa mapokezi aliyopata
 Filipe Nyusi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
   Mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji akiwa na Mwenyeji wake, Kinana wakati wa mapokezi yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
   Mama Maria Nyerere akimsalimia Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Machel, Samora Samora ambaye alifuatana na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji.

No comments: