Tuesday, March 30, 2010

Vodacom yamwaga kompyuta mashuleni Singida


Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack akiangalia jinsi kompyuta inavyofanya kazi baada ya kukabidhiwa rasmi kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za sekondari ya Shului na Isuna zote za Iramba anaeangalia kushoto Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mshamu Manyinja na Alice Mlumba.

Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.

*************************************************************************************

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 pamoja na kuunganisha mtandao wa internet kwa shule mbili za Sekondari ya Shelui na Isuna zilizoko Lindi Vijijini ili kuboresha sekta ya Elimu katika shule hizo.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Meneja wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule alisema kwamba msaada huo ni mwendelezo wa awamu ya tatu ya Mradi wa Ugawahi kompyuta kwa shule za sekondari za vijijini. Katika awamu ya kwanza na ya pili jumla ya shule 30 kutoka mikoa tofauti 15 zilifaidika katika mradi huu.

Alisema huu ni mwanzo tu kwani Vodacom Foundation itaendelea kutoa misaada ya kompyuta katika shule za mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa unalenga kutoa wimbi la uduni wa Teknologia ya kompyuta na kuinua elimu na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee lazima tuwe pamoja kuendeleza misingi iliyobora ya elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo na kusema sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi wanaopatwa na upungufu wa vitu muhimu katika jamii.

“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’

Alisema hivi sasa bila teknolojia ya kisasa amna maendeleo na alichukua frusa hiyo ya kuwaasa wanafunzi wazitunze kompyuta hizo na kuzitumia vizuri kwani mpo sambamba na shule zailizoko mjini sasa.

No comments: