Monday, March 15, 2010

Mpango maalumu kuwezesha wanafunzi



Mkurugenzi wa Mtendaji wa kampuni ya 4Layers Tuition Management Solution Nashesha Mvungi ,akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa mpango maalum wa kuwawezesha wanafunzi wa ngazi zote kupata nafasi ya kusoma ndani ya Nchi bila kujali jenda na pointi za masomo,mpango huo ambao umeandaliwa na kampuni ya 4Layers unajulikana kwa jina la NITASOMA Scholarships, kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (tpsf) Esther Mkwizu.Picha na Michael Matemanga.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (tpsf) Esther Mkwizu(kushoto),akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa mpango maalum wa kuwawezesha wanafunzi wa ngazi zote kupata nafasi ya kusoma ndani ya Nchi bila kujali jenda na pointi za masomo,mpango huo ambao umeandaliwa na kampuni ya 4Layers unajulikana kwa jina la NITASOMA Schola rships,kulia ni mkurugenzi wa Mtendaji wa kampuni ya 4Layers Tuition Management Solution Nashesha Mvungi.Picha na Michael Matemanga.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX



Mama mleziwa NITASOMA Scholarship scheme mheshimiwa mama Esther Mkwizu, wageni waalikwa toka Wizara ya Elimu, Tanzania Commision of Universities, The Gaming Board of Tanzania, Push Mobile, Goethe Institute, Macmillan, Ndugu zangu waandishi wa habari, ndugu wanafunzi wa wakilishi wa vyuo mbalimbali wageni waalikwa mabibi na mabwana.

Kwa niaba ya uongozi wote wa kampuni ya 4layers (T) Ltd, napenda kuwashukuruni sana kwa kujumuika nasi siku hii muhimu sana kwetu sisi kama kampuni. Siku ya uzinduzi wa huduma maalum kwa jamii NITASOMA.Kampuni ya 4Layers (T) Ltd, Tuition Management Solution inaazisha mpango maalum wakuwawezesha wanafunzi katika ngazi zote kupata nafasi ya kusoma ndani ya nchi bila kujali, jenda, rangi, kipaji, wala alama za juu za masomo, ujulikanao kwajina la NITASOMA Scholarships for NON and Merit Students.

4Layers (T) Ltd ni miongoni mwa kampuni chache nchini ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma hususani katika maswala ya Elimu.Ndugu waandishi wa habari ,kwa wanafunzi walengwa mpango huu utaanza rasmi tarehe 15.03.2010 , huduma ambazo kampuni hii itatoa ni scholarship kwa mashule na vyuo taasisi zote za elimu ya juu kwa ujumla vilivyopo nchini,
Pili ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wanafunzi juu ya kuchagua masomo kwa shule za sekondari pia kuelimishwa jinsi kujiunga na mashule au vyuo na vitengo mbalimbali vya elimu na ufundi, mafunzo katika kuandika barua ya kuomba kazi , muongozo kamili katika kuboresha elimu kwa ujumla huduma hii itawalenga wanafunzi kuanzia shule za sekondari, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu.

NITASOMA Annual Career day ni siku ambayo wanafunzi watakutana na wataalam maarufu nchini ana kwa ana na kujadiliana kuhusu ubora, umuhimu hata matatizo ya ufanisi katika sekta hizo mbalimbali.Nimatarajio yetu pia katika siku za mbele ni kutoa udhamini katika shughuli mbalimbali za kielimu na vijana.

Nikiwa kama Mkurugenzi Mtendaji , napenda kufafanua kuwa kipindi cha mwaka tunatarajia kusomesha bure wanafunizi 6 kwa muda wote wa masomo na kutoa zawadi za Laptop 12, vitabu vya masomo au vifaa vya masomo kwa wanafunzi 12, simu ya mkononi 1 kwa wiki zawadi hizi ni kwa wanafunzi wale watakaoshinda kupitia bahati nasibu maalum.

Wanafunzi watakao kufaidika na mpango huu ni wale tu watakao tuma ujumbe mfupi wa simu NITASOMA SEC au NITASOMA HIGH kwa shule za sekondari au NITASOMA UNI kwa vyuo vikuu kwenda kwenye namba 15767 na ataingia katika mchakato huo kwa gharama ya shilingi ya kitanzania 500 tu.Zawadi hizo zitatolewa kwa awamu yaani laptop moja kwa kila mwezi. Simu ya mkononi kila wiki na vitabu kila mwezi tukizingatia masharti na vigezo.

Kuhusiana na utaratibu wamalipo, 4 Layers (T) Ltd Tuition Management solutions kama kampuni itafanya malipo moja kwa mojakatika shule au chuo husika haku na mwanafunzi atakayepewa ada ya masomo (Tuition fees)fedha za vitabu mkononi.Nimatarajio yetu kuchagua mshindi wa kwanza wa NITASOMA Scholarship kwa zawadi ya simu ya mkononi tarehe 22.03.2010 yaani jumatatu ijayo.

watembelee katika mtandao wao
www.nitasoma.com

No comments: