Monday, March 01, 2010

Breaking Newss watu 24 wafa ajali ya basi

Habari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa 24 wamekufa papo hapo na wengine 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea jana jioni eneo la mpaka kati ya Nzega na Igunga mkoani Tabora.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10: 15 jioni katika vijiji vya Kitangili na Migua baada ya basi aina ya Scania lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mwanza kupinduka.

Waliokufa ni wanaume 14, wanawake sita na watoto wanne huku majeruhi ni wanaume 35, wanawake kumi na watoto 7 huku majeruhi wanne wamepelekwa katika Hospitali ya Bungando mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi.

Mganga wa wilaya ya Nzega, Dk John Mwombeki alisema maiti pamoja na majeruhi hao wapo katika hospitali ya Nzega. Taarifa zaidi tutawaleteeni baadaye.

No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...