Tuesday, March 30, 2010

JK apokea misaada toka China


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam leo asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepanda katika pikpiki aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xingshen kama seshemu ya msaada wa China kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Misaada mingine iliyokabidhiwa katika hafkla hiyo ni pamoja na baiskeli, chupa za maji na mashine za kushonea nguo.

Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro.

No comments: