Rais wa Zamani wa Zanzibar afariki Dunia leo, Rais Dkt. Magufuli atuma salamu za rambirambi


Taarifa iliyotufikia mchana huu, inaeleza kuwa  kuwa Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi (1972-1984), Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. 
Mzee Aboud Jumbe amefikwa na mauti hayo nyumbani kwake Kigamboni, Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri wa Muungano amemtumia Salaam za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa msiba huu mzito

Comments