Wachezaji wa Timu ya Azam pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Mgeni Rasmi katika Mtanganye wa kuwania Ngao ya Jamii uliozikutanisha Timu ya Azam na Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Azam, John Boko 'Adebayour', baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Beki wa Timu ya Azam FC, David Mwantika akizua mpira kwa umaridadi mkubwa huku akimdhibiti Mshambuliaji machachari wa Yanga, Donald Ngoma katika mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kulingana 2-2, na kupelekea kuamuliwa kupigwa mikwaju ya penati iliyoipa ushindi timu ya Azam kwa mabao 4-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akitaka kuzuia shuti la Beki wa Azam, Shomari Kapombe.
Kipa wa Azam akiwa chini huku mpira ukiwa wavuni, baada ya kupelekwa markiti na Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma kwa mkwaju wa penati.
Beki wa Yanga, Hassan Kessy akiutuliza mpira kwa ustadi mbele ya Benchi la Wapinzani wake.
Comments