WAZIRI WILLIAM LUKUVI ATEMBELEA NYUMBA ZILIZOHAMISHIWA UMILIKI TOKA SHIRIKA LA NYUMBA KWENDA SERIKALI ZA MITAA MKOANI IRINGA
Waziri alikusudia kuona hali alisi ya nyumba zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ili kupata taswira ya nyumba zote zilizoko Mikoa mingine na kutoa taarifa ya Mheshimiwa Rais juu ya mustakali wa nyumba hizi.
Waziri Lukuvi,
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa William Donald Mafwele alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baada ya hapo msafara uliojumuisha watendaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wa Mkoa Iringa ulielekea eneo la barabara ya Kalenga kuliko na nyumba 49. Mheshimiwa Waziri alifanya ukaguzi wa eneo hilo na kumuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri, William Donald Mafwele kuhusu hali ya umiliki ulivyo sasa. Baada ya hapo msafara wa Waziri ulielekea eneo la Barabara ya Pawaga kuliko na nyumba 25.
Wapangaji waliopanga kwenye nyumba zilizokuwa za NHC na kukabidhiwa kwa Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi (hayuko pichani) kwenye ukumbi wa Mwembetwoga mkoani Iringa.
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba Taifa mkoani Iringa, Repson Yosia akisoma taarifa mbele ya Mheshimiwa Waziri.
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Iringa akimkabidhi taarifa Mheshimiwa Waziri.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, William Donald Mafwele akisoma taarifa mbele ya Mheshiwa Waziri.
Comments