Tuesday, August 02, 2016

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa
uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani
uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo
kupitia kampeni yake ya “Be Kidotified”.  Mjema alizindua uwanja huo leo
katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate
akishuhudia tukio hilo.
PICHA NA MICHUZI JR
 Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa
shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto)
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia
kampeni yake ya “Be Kidotified” uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa
pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule
Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa. 
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
 
 Mandhari ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya
Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya
“Be Kidotified”.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla
fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
……………………………………………………….
 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya “Be Kidotified”. Alisema kuwa
amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya
kuendeleza michezo na taaluma.
Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia
jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja
utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli)
kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani. 
Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule
hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa
serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi
milioni 50.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya
michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya
sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha
zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini. 
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa
changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya
michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo
vitamwezesha mshiriki kupata ajira. 
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo
nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi
kuonyesha vipaji vyao ipasavyo. 
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo,
lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje
ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi. 
“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo
nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi
wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ” 
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation,
na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be
Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule
nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate. 
Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini
katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa
upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu. 
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na
kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti
brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli
mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila
siku.
Post a Comment