PROFESA MUHONGO AZINDUA MPANGO MKUBWA WA KUENDELEZA USAMBAZAJI UMEME VIJIJI VYOTE TANZANIA WENYE THAMANI YA DOLA 1,367


Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati akizindua mpango mkubwa wa kuendeleza usambazaji umeme vijijini hapa nchini (Treep), kwenye kijiji cha Kwedizinga, wilayani Handeni mkoa wa Tanga agosti 15, 2016. kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawai na Somalia, Bella Bird (PICHA NA MARGRETH SUBI)

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawai na Somalia, Bella Bird, (kushoto waliokaa) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Gessima Nyamo’hanga, wakisaini makata wa makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo wa TREEP, mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo kwenye hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa mpango huo.

NA MAGRETH SUBI

WAZIRI wa Nishati na Madini Mh. Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mpango mkubwa wa kuendeleza usambazaji umeme vijijini hapa nchini, (Tanzania Rural Electrification Expansion Program- TREEP” katika kijiji cha Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga.

Sambamba na uzinduzi huo uliofanyika Agosti 15, 2016, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bi. Bella Bird, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Gissima.Nyamo’hanga, walisaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mpango huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo utakaogharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 1,367, Profesa Muhongo alisema, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi wake, Rais John Pombe Magufuli, imedhamiria kuwafikishia umeme wananchi walio vijijini ili hatimaye uwawezeshe kuinua vipato vyao kutokana na kutumia Nishati ya umeme katika shughuli zao za kila siku.

Mpango huo utakaonufaisha vijiji vyote nchini na ambao unafadhiliwa na wadau wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia, (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Misaada la Maendeleo la Sweden (SIDA), Shirika la Misaada ya Kimaendeleo la Norway, (Norad), na Jumuiya ya Ulaya, (EU), KFW, GIZ, JICA, utakamilika mwaka 2022. 

Profesa Muhongo aliwashukuru washirika wa maendeleo, kwa kuendelea kufanya kazi pamoja na serikali, katika kutatua changamoto mbalimbali.

“Dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kujenga uchumi wa kati, na ili kufikia azma hiyo lazima wananchi wapate umeme na hii ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magifuli kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa viwanda.” Alisema.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati ya Umeme vijijini (REA), ambao ndio wasimamizi wa mradi huo, Bw.Gideon Kaunda aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi huo ili kuharakisha kukamilika kwake.

Akimkaribisha Mh. Waziri wa Nishati na Madini kuzindua mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigella, aliwataka wakazi wa mkoa huo, kuchangamkia fursa hiyo ya upatikanaji wa umeme kwa kuanzisha miradi mmbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogovidogo. “Niwaombe ndugu wananchi, sasa tufanye kazi kwa bidii ili tujiletee maendeleo yetu,” alsema Mh. Shigella.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Nishati Vijijini, (REA), Mhandisi Gissima Nyamo'hanga alisema mradi huo wa TREEP utachangia pakubwa kuwaongezea kipato wanavijiji kwa kuboresha miradi yao na kuanzisha miradi mipya inayotegemea umeeme kama uanzishaji wa viwanda vidogovidogo na hivyo kuwaletea maendeleo watanzania waishio vijijini.

Mh. Profesa Muhongo, Washirika wa Maendeleo, vingozi wa Mkoa wa Tanga, Wabunge na Viongozi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na wale wa REA na viongozi wa kijiji, wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, akitoa muhtasari wa shughuli ya uzinduzi wa Mpango huo na kumkaribisha mgeni rasmi, wadau wa maendeleo na wananchi
Baadhi ya wageni walioshiriki kwenye uzinduzi huo

Comments